Ligi kuu Tanzania Bara maarufu kama Vodacom inatarajiwa kuendelea tena leo kwa mchezo utakaowakutanisha Mbeya City ya Jijini Mbeya dhidi ya Yanga ya jijini Dar-Es-Salaam. Yanga inaingia katika mchezo huu ikiwa tayari imeshajihakikishia ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara msimu wa 2015/16 baada ya Simba kupoteza mchezo wake dhidi ya Mwadui FC,mechi hiyo inatarajiwa kuwa kali na ya kuvutia licha ya Yanga kuwa mabingwa tayari kutokana na ushindani uliopo baina ya timu hizi, Mbeya City inahitaji ushindi katika mchezo huo ili kujihakikishia kubaki kwao katika ligi kuu msimu ujao.
0 comments:
Post a Comment