Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara timu ya Yanga SC, wanatarajiwa kupewa kombe lao la ligi kuu msimu huu katika mchezo wao dhidi ya Ndanda FC utakaofanyika katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, sherehe hizo za kukabidhiwa kombe vijana wa jangwani zilitarajiwa kufanyika leo katika mchezo wao na Mbeya City lakini kwa maelezo ya TFF ni kwamba wamechelewa kufanya maandalizi ili kuwezesha sherehe hizo kufanyika leo badala yake zitafanyika katika mechi kati ya mabingwa hao na Ndanda Fc utakaofanyika May 14/2016.
0 comments:
Post a Comment