Tuesday, May 10, 2016

WACHEZAJI SIMBA WAGOMA KUCHEZA NA MAJIMAJI


Hali ya sintofahamu imezidi kuimkumba klabu ya Simba, baada ya wachezaji wake 7 kususia mechi kati yao na Majimaji ya Songea itakayochezwa siku ya Jumatano May 11. Wachezaji hao sita ni wakigeni na mmoja ni wa ndani, wachezaji  6 wa kigeni waliogoma kusafiri kuifuata Majimaji ni mlinda mlango Vincent Angban (Ivory Coast), mabeki Emery Nimubona (Burundi), Juuko Murshid (Uganda), viungo Justice Majabvi (Zimbabwe), Brian Majwega (Uganda), Hamisi Kiiza (Uganda).Hamisi Kiiza nae akiwemo katika orodha hiyo.

Kiungo  Mwinyi Kazimoto ni mchezaji wa ndani ambae nae pia amegoma kusafiri na timu kuelekea mkoani Ruvuma kucheza na Majimaji, sababu ya wachezaji hao wote kugoma ni kucheleweshewa mishahara yao ya mwezi wa nne.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Hajji Manara,amesema sababu ya kuchelewa kwa mishahara ya wachezaji hao inatokana na wadhamini wao Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kuchelewa  kuwapatia fedha za udhamini.

0 comments:

Post a Comment