Klabu Bingwa Afrika Mashariki na kati Azam FC ilikuwa ugenini jijini Tanga kupambana na African Sports katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara maarufu kama Vodacom. Azam FC wamefanikiwa kuibuka na ushindi katika mchezo huo wa jumla ya magoli 2 - 1. Magoli ya Azam FC yamefungwa na Allan Wanga dakika ya 10 na Erasto Nyoni dakika ya 74, huku goli pekee la African Sports likiwekwa kimiani na Omary Ibrahim katika dakika ya 11.
Matokeo haya yameifanya Azam FC kuendelea kushikilia nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi kwa kufikisha pointi 63 katika michezo yao 29.
0 comments:
Post a Comment