Saturday, February 18, 2017

Simba yajifua Zanzibar kuelekea february 25


Timu ya Simba jana imeondoka kwenda visiwani Zanzibar kujiandaa na mchezo wake wa February 25 dhidi ya watani zao wa jadi Yanga.

Simba ambayo ndio inayoongoza ligi kwa kujikusanyia point 51 katika michezo 22, watani zao Yanga wao wapo nafasi ya pili baada ya kushuka uwanjani mara 21 na kujikusanyia pointi 49.

Simba ambayo inajiwinda pengine iweze kuondoa mkosi wa kukaa nje ya mashindani ya kimataifa yanayotambuliwa na shirikisho la soka barani Afrika kwa takribani miaka minne mfululizo, wanafanya mazoezi asubuhi na jioni kwa kusuduo la kuwaweka sawa wachezaji wao kisaikolojia na kimbinu ili kuhakikisha wanaimaliza Yanga.

Simba ambayo jana imetoka kuitoa Africans Lyon katika kuwania kombe la shirikisho Tanzania na badae walianza safari ya kuelekea Kisiwani.

Huenda mchezo huo ukatoataswira ya timu gani itakuwa bingwa msimu huu.

Yanga na Azam ndio timu ambazo kwa miaka minne mfululizo zinapata tiketi ya kupanda ndege kwenda kwenye mashindano makubwa ya bara la Afrika yaani Kombe la shirikisho na kombe la mabingwa kwa ngazi ya vilabu.

Msimu uliopita timu ya Yanga ilibahatika kutinga katika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho na kushika mkia katika kundi lake.

Kitu kizuri kwa upande wa simba nikuwa Hakuna majeruhi.


0 comments:

Post a Comment