Saturday, February 11, 2017

Simba yarudi kileleni, yaitumia salamu yanga february 25



Mpira ulianza kwa kasi na 11’ alimanusura Benjamin Asukile aifungie Prisons goli pale kichwa chake kilipoenda pembeni kidogo mwa lango la simba baada ya kazi nzuri ya Mohammed Samatta.

Juma Luzio mchezaji wa Zesco United ya Zambia anaecheza kwa mkopo Simba na Ibrahim Ajib walihakikisha simba inaenda mapumziko ikiwa mbele kwa 2 – 0.

Ilichukua dakika 18 tu tangu kuanza kwa mchezo, Luzio aliiandikia simba goli la kwanza baada ya kumalizia kazi nzuri ya beki wa kulia wa timu simba Janvier Besala Bokungu.

Dakika kumi 28’badae Ibrahim Ajib aliweka goli la pili baada ya Mavugo kufanya kazi ya ziada na kumpa nafasi mfungaji ambae aliukwamisha kimiani mpira bila ajizi
Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika Simba 2 – 0 Tanzania Prisons .

Kipindi cha pili dakika ya 67 Mavungo alimalizia krosi safi toka kwa Ibrahim Ajib na kuipatia Simba goli la 3.

Alimanusura Kichuya afunge goli pale shuti lake lilipogonga mwamba na kurudi uwanjani na kumkuta mavugo aliepoteza nafasi hiyo.

Mpaka firimbi ya mwisho inapulizwa Simba 3 – 0 Tanzania Prisons, na kurudi kileleni baada ya kufikisha pointi 51 baada ya michezo 22, huku yanga wao wakicheza michezo 21 na kufikisha pointi 49.

Mchezo ujao wa simba ni February 25 watakapokutana na watani zao wa jadi Yanga.

Ndanda 0 - 0 Toto africa

Stand UTD 0 - 0 Majimaji

mchezo mwingine ulipigwa katika dimba la mabatini mkoani pwani kati ya Ruvu Shooting walitoka sare ya bila kufungana na mabingwa wa Afrika mashariki na kati(Kagame Cup) timu ya Azam Fc

0 comments:

Post a Comment