Ukiwa ni mchezo wake wa 16 mfululizo bila kupoteza katika
ligi kuu ya uingereza timu ya Manchester united imeichapa Watfod 2 – 0 na kupunguza gepu
kuwania kuingia katika timu nne za juu(Big Four)
Mchezaji bora wa mchezo wa leo Anthony Martial
alimtengenezea nafasi kiungo mtafutaji Juan Mata 32’ na Mata akaukwamisha mpira
wavuni na kuwaamsha Washabiki waliojaa katika majukwaa ya Old Trafford.
Juan Mata
60’ Anthony Martial alimalizia kazi nzuri iliyofanywa na
mkongwe Zlatan Ibrahimovic na kuiandika UTD goli la pili.
Anthony Martial
Mchezo wa leo nusura
uishe bila kadi yoyote lakini Antonio Valencia alipewa kadi ya njano 90’.
Hadi mpira unamalizika UTD 2 – 0 Watfod, baada ya mchezo huo
UTD wamefikisha point 48, point 2 nyuma ya Tottenham na Arsenal wanaoshika
nafasi ya 2 n 3.
Pamoja na ushidi huo bado Man U wanabaki katika nafasi yao
ya 6 ambayo imekuwa ni ngumu kwao kuikimbia kwa muda mrefu sasa.
Matokeo mengine ni kama yanavyoonekana
Middlesbrough 0 - 0
Everton
West Ham United 2 - 2 West Bromwich Albion
Sunderland 0 - 4 Southampton
Stoke City 1 - 0 Crystal Palace
0 comments:
Post a Comment