Magoli mawili ndani ya dakika mbili yaliyofungwa na
Msenegali Sadio Mane yameiwezesha Liverpool kufikisha point 49 nyuma ya Chelsea
yenye 59, Tottenham na Arsenal zote zikiwa na 50 kila moja.
Dakika ya 16 Georginio Wijnaldum alimtengenezea nafasi Sadio
Mane nae bila ajizi akaukwamisha mpira kwenye goli la Tottenham .
18’ Sadio Mane tena alijetenga na kumalizia mpira
uliookolewa na kipa wa Tottenham baada ya shuti kali la Adam Lallana na kuipa Liverpool
uongozi wa 2 – 0 mpka mapumziko.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi Tottenham wakijaribu
kukomboa na Liverpool wakijaribu kuongeza lakini mpaka 90’ Matokeo yakabaki Liverpool
2 – 0 Tottenham.
Wachezaji watano wa Tottenham walionyeshwa kadi za njano
ambao ni: Heung-Min Son 28’, Harry Kane 67’, Harry Winks 71’, Eric Dier 78’ na Toby
Alderweireld 83’
Wachezaji watatu wa Liverpool nao walionywa kwa kadi za
njano: Jordan Henderson 53’, Joel Matip
56’, James Milner 68’.
Vikosi
Liverpool :
Simon Mignolet, Nathaniel Clyne, James Milner, Lucas Leiva(82’),
Joel Matip, Adam Lallana, Jordan Henderson, Georginio Wijnaldum, Sadio Mane(90’),
Roberto Firmino, Philippe Coutinho 77’
substitutions:
Emre Can 77’, Ragnar Klavan 82’, Trent Alexander-Arnold 90’ Loris
Karius, Daniel Sturridge, Alberto Moreno, Divock Origi
Kocha: Jurgen Klopp
Tottenham :
Hugo Lloris, Kyle Walker, Ben Davies, Toby Alderweireld, Eric
Dier, Victor Wanyama, Moussa Dembele77’, Christian Eriksen 68’, Dele Alli, Heung-Min
Son 82’, Harry Kane
substitutions:
Harry Winks 68’, Moussa Sissoko 77’, Vincent Janssen 82’, Georges
N'Koudou, Kieran Trippier, Kevin Wimmer
Kocha: Mauricio Pochettino
0 comments:
Post a Comment