Sunday, February 12, 2017

Alves 0 -6 Barcelona, Suarez aongoza mauaji hayo, Madrid nayo ni moto wa kuotea mbali



Suarez ametupia mara mbili na kutengeneza mengine mawili katika mchezo wa ligi kuu ya Hispania maarufu kama “Spain - LaLiga Santander”

Katika mchezo huo wa jana Barcelona wakicheza kwa nguvu na kujiamini muda wote iliwachukua dakika 37 kujipatia goli la uongozi pale Ivan Rakitic alipompenyezea mpira Aleix Vidal ndani ya eneo la penati, nae Vidal akamtangulizia Luis Suarez na kuipa timu yake goli hilo.

Makosa ya beki Fernando Pacheco yaliigharimu timu yake 40’ pale aliposhindwa kuondosha mpira ambao ulitua kichwani mwa Suarez kabla ya kumkuta Neymar alieukwamisha wavuni


Mpaka timu zinakwenda mapumziko Alaves 0 – 2 Barcelona.

Kipindi cha pili kiliendelea kuwa cha upande mmoja zaidi na 59’ Lionel Messi aliipa Barcelona uongozi wa 3 – 0 baada ya makosa ya beki Carlos Vigaray na kusababisha Messi kubaki yeye na kipa.

63’ Alexis alijifunga katika harakati za kuokoa mpira uliokolewa na mlinzi mwenzake na kumgusa kasha kuiandikia Barcelona goli la 4.

Pasi nzuri toka kwa Suarez ilikutana na - Ivan Rakitic na kuiandikia Barcelona goli la 5.
Goli la 6 liliwekwa kimiani na Suarez baada ya kipa kutema mpira uliopigwa na Neymar.

Mpaka 90’ zinamalizika Alaves 0 – 6 Barcelona.

kwa Matokeo haya Barcelona wamebaki nafasi ya pili baada ya michezo 22 na kujikusanyia pointi 48 nyuma ya Real Madrid yenye pointi 49 kwa michezo 20

Matokeo ya michezo mingine :
Real Betis 0 - 0 Valencia
Athletic Bilbao 2 - 1 Deportivo La Coruna

Osasuna 1 - 3 Real Madrid

Magoli ya Madrid yalifungwa: Cristiano Ronaldo 24’, Isco 62’ na Lucas Vazquez 90’

Goli la Osasuna lilifungwa: Sergio Leon 33’

0 comments:

Post a Comment