Ikiwa imetoka
kusuluhu na Liverpool, Chelsea itataka kujihakikishia nafasi ya kutwaa
kombe pale tu itakapoweza kupata Matokeo chanya mbele ya Arsenal
Arsenal inaingia uwanjani Stamford Bridge kwa lengo moja la
kuhakikisha inapunguza gepu la pointi na kufikia 6.
Mechi ya mwisho ya Epl Arsenal walikubali kipigo cha 2 -1
kutoka kwa Watford, wakati Chelsea wao walitoka sare ya 1 -1 na Liverpool .
Mchezo wa mwanzo uliozikutanisha Arsenal na Chelsea, Arsenal
walitungua Chelsea 3 -0 katika dimba la Emirates magoli ya Alexis Sanchez, Theo
Walcott na Mesut Ozil, hvyo leo Chelsea watahitaji kulipa kisasa ndani ya uwanja
wao huku Arsenal wakitaka kulinda Heshima yao mbele ya Chelsea.
Mchezo huo utaanza saa 15:30 kwa saa za Afrika Mashariki.
0 comments:
Post a Comment