Saturday, February 4, 2017

Serengeti Boys hiyooo AFCON U17, 2017

                                                          Serengeti Boys
Akizungumza na TBC waziri wa michezo Mh Nape Nnauye alisema Serengeti Boys wameshinda rufaa yao na hivyo watashiriki Mataifa ya Afrika mapema mwaka huu.
                                              Langa-Lesse Bercy
Ni furaha ndermo na vifijo kwa watanzania wote na afrika mashariki yote baada ya shirikisho la soka Afrika(CAF) kupitia kamati yake tendaji  kuipa ushindi timu ya taifa ya vijana serengeti Boys katika kesi ya kupinga umri wa kijeba wa timu ya U17 ya Congo Brazzaville Langa-Lesse Bercy

Ikumbukwe srengeti boys ilitolewa na Congo kwa faida ya goli la ugenini, mchezo uliofanyika Dar es salaam boys waliitandika Congo 3-2 na mchezo wa marudiano Congo waliibuka na ushindi wa 1- 0
Serengeti boys imeweka kambi katika hostel za TFF karume jijini Dar es salaam kujiandaa na mashindano hayo

Related Posts:

  • SIMBA YAPEWA ONYO MBEYA Timu ya soka ya Simba inatarajiwa kushuka katika dimba la Sokoine Jijini Mbeya siku ya jumatano kuvaana na timu ya wananchi kutoka jijini humo Mbeya City. Kuelekea Mchezo huo, Klabu ya Mbeya City imetoa onyo kwa Wekundu h… Read More
  • MCHEZO WA STARS NA ETHIOPIA WAYEYUKA Lile pambano lililokuwa linasubiriwa kwa hamu na wapenzi wengi wa soka nchini limeota mbawa baada ya shirikisho la soka la Ethiopia kuiandikia TFF kuwa mchezo huo hautakuwepo kutokana na sababu za kiusalama nchini Ethiopia… Read More
  • MARUFUKU SIMBA NA YANGA KUTUMIA UWANJA WA TAIFA Serikali yatoa katazo juu ya simba na yanga kuuutumia uwanja wa taifa na kuwaambia watafute pakuchezea mechi zao. Hayo yamesemwa na waziri anaehusika na michezo mheshimiwa Nape.Nape alisema hivi “Uwanja huu sasa hautatumik… Read More
  • TAARIFA YA YANGA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KUKODISHA TIMU TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI MUHTASARI WA MKATABA.  1. Bodi ya Wadhamini wa Young Africans Sports Club, (ambayo hapa inajulikana kama Mmiliki”) imeingia tarehe 3 September, 2016 Mkataba wa kukodishwa na kampuni iju… Read More
  • VIONGOZI TOTO AFRICANS WATUMBULIWA Uongozi wa klabu ya Toto Africans ya jijini Mwanza umewasimamisha baadhi ya viongozi wake kutokana na kile kilichotajwa kuwa ni utovu wa nidhamu. Godwin Aiko, Mwenyekiti wa klabu hiyo amesema sababu kubwa ya kuwasimamisha… Read More

0 comments:

Post a Comment