KRC Genk leo inashuka katika dimba lake la nyumbani la
Luminus Arena kumenyana na timu inayoburuza mkia katika Belgium - Pro League timu
iitwayo Royal Excel Mouscron. Mchezo utakaopigwa saa 22:00 majira ya Afrka
Mashariki.
Genk ipo nafasi ya 8 baada ya michezo 23 ikiwa na alam 34.
Genk ipo nafasi ya 8 baada ya michezo 23 ikiwa na alam 34.
Mchezaji Mbwana
Samatta ambae anaiwakilisha vyema Tanzania kimataifa kwa sasa, yupo nafasi ya
15 pamoja na kiungo mshambuliaji wa Manchester City Kevin De Bruyne kwa
upachikaji mabao katika historia ya KRC Genk kwa kutia kambani jumla ya magoli
17 huku anaeongoza akiwa na magoli 105 ambae anaitwa Jelle Vossen.
Hii ina maana kuwa endapo Samatta atafunga goli tatu leo
atakuwa sawasawa na Christian Benteke ambae anakipiga katika klab ya Crystal
Palace.
Kilalakheri Samatta katika mafanikio yako Watanzania tupo
nyuma yako.
0 comments:
Post a Comment