Monday, February 6, 2017

Leicester yakubali yaishe kwa Man U, yatota 3 - 0


King Power Stadium
Ikicheza kwa kujiamini muda wote Manchester United imeitandika Leicester-city bila huruma goli 3 – 0 katika dimba la King Power huko Leicester.

Ilibidi united wasubiri mpka dakika 41 ndio waanze kufungua ukurasa wa mabao pale mchezaji hatari anaerudi kwenye kiwango chake bora kabisa Henrik Mkhitaryan kutikisa wavu kiufundi.
Wakati Leicester wakitafakari jinsi ya kuchomoa na kuongeza ghafala Zlatan Ibrahimovic aliwaamsha mashabiki wa united mnamo dakika ya 44’ kwa kuipatia united goli la pili.

Mpaka mapumziko  Leicester-city 0 – 2 Manchester United huku Manchester wakiwa wamepiga mashuti mengi langoni mwa Leicester.
Kipindi cha pili tulishudia rafu nyingi na kusababisha wachezaji kadhaa wa united  kulimwa kadi za njano.
49’ Juan Mata alihitisha ushindi huo wa 3 – 0 ambao huenda ikawa ndio mwanzo mzuri wa kuanza kuitafta big four.
Kadi za njano
Leicester city: Danny Drinkwater 5’, Christian Fuchs 40’
Man United: Juan Mata 28’, Ander Herrera 55’, Paul Pogba 56’, David De Gea 88’.
possession (%)
Leicester city: 32

Man United: 68

0 comments:

Post a Comment