Monday, February 6, 2017

16 Bora Azam Federation Cup ratiba yatangazwa, michezo 8 kufanyika kwa siku tatu tofauti


Michuano ya kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) hatua ya 16 bora kutimua vumbi February 24 na February 26 na march 7 katika mikoa sita ya Tanzania Bara.
February 24 kutakuwa na michezo minne katika mikoa minne tofauti
Mkoani Arusha
Katika dimba la Sheikh Amri Abeid wenyeji timu ya Madini Fc watawakaribisha maafande wa JKT Ruvu
Mkoani Dar es Salaam
Mabingwa wa Afrika Mashariki na kati Azam Fc watailika timu ngumu ya Mtibwa Sugar katika dimba lao la nyumbani (Azam Complex, Chamaz).
Azam  ndio makamu bingwa wa michuano hiyo kwa msimu uliopita baada ya kupokea kichapo cha goli 3 – 1 kutoka kwa Yanga.

Mkoani Kagera

Timu ya Kagera sugar wataikaribisha timu ya Stand United katika dimba Kaitaba.

Mkoani Ruvuma

Timu za Mighty Elephant mkoani humo itawaalika wanakuchele Ndanda kutoka Mtwara katika Uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Raundi hiyo ya 16 itaendelea tena siku ya jumapili February 26 katika mikoa mitatu.
Mkoani Dar es Salaam

Timu ya Simba itavaana na timu African Lyon katika dimba la Uwanja wa Taifa.

Mkoani Mwanza

Kutakuwa na Mwanza derby wakati Mbao FC itakapoonyeshana ubabe na kaka zao Toto Africans katika Uwanja wa CCM Kirumba
Mkoani Mbeya

Derby nyingine itakuwa mkoani Mbeya wakati timu mbili za mkoani humo Tanzania Prisons na Mbeya City zitakapomenyana kuwania kuingia roba fainali ya michuano hiyo

March 7


Mabingwa wa michuano hiyo kwa msimu uliopita timu ya Yanga wao wataialika timu ya Kiluvya kutoka mkoani pwani katika dimba kuu la Uwanja wa Taifa jiji Dar es Salaam

bingwa wa michuano hii ndie atakaeiwakilisha Tanzania katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika 2018.

0 comments:

Post a Comment