Kocha mkuu wa zamani wa klabu ya Mwadui ya mjini Shinyanga, Jamhuri Kihwelu, ameweka bayana kuwa yupo tayari kurudi kuitumikia Simba katika nafasi ya ukatibu mkuu.
Julio amesema kuwa hana wasiwasi na yupo tayari kuitumikia klabu hiyo endapo tu uongozi wa Simba utaridhia kumpa nafasi hiyo.
"Siyo kama najipigia chapuo lakini kama viongozi wa Simba wakiamua kunipa nafasi ya ukatibu sitaweza kukataa kwa sababu naipenda timu hiyo na kila mmoja anajua na kama nikiwepo naamini nitaongezea kitu fulani na kuifanya timu ipate matokeo mazuri"
Nafasi hiyo ilikuwa inashikiliwa na Patrick Kahemela ambaye kwa sasa amekuwa mkurugenzi wa michezo katika kituo cha runinga cha Azam. Aidha, Julio ameongeza kuwa, uzuri wake yeye ni kwamba hakufungiwa na mtu yeyote kujihusisha na mpira wa miguu isipokuwa ni yeye mwenyewe tu ndiye aliamua kukaa pembeni kutojihusisha na maswala hayo.
“Uzuri wangu kwangu kwamba sikufungiwa na mtu yeyote kujihusisha na soka hivyo hata nikirejea hakuna ambaye atashtuka na niwaahidi kwamba nitaitumikia nafasi hiyo kuleta mabadiliko yaliyoshindikana kwa kipindi kirefu,” alisema Julio akizungumza na Championi

0 comments:
Post a Comment