Wednesday, February 8, 2017

Mkongwe Chelsea Amchana John Terry

Marcel Desailly beki wa zamani wa Chelsea amemwambia John Terry kwamba muda wake umekwisha Chelsea.

Desailly anaaamini kuwa muda wa Terry kuondoka Chelsea umewadia na ni kutokana na kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Mtaliano Antonio conte.

"Terry si beki kisiki tena kwenye kikosi cha kwanza Chelsea chini ya Antonio Conte akiwa ameanza mechi tano tu Ligi Kuu msimu huu."

Aidha Mkongwe huyo wa zamani wa Chelsea ameongeza kuwa, yeye aliondoka klabuni hapo baada ya kuona kuna wachezaji wenye uwezo na kasi zaidi yake akaona ni wazi kuwa muda wake wa kuondoka ulikuwa umewadia.

"Niliondoka kwa sababu kulikuwa na wachezaji wenye kasi zaidi yangu, bora kuliko mimi na ulikuwa muda wangu wa kuondoka – muda wao wa kung’ara – na sasa ni muda wake,” Desailly alikiambia Sportsmail.

Licha ya kumwambia Terry afungashe virago vyake hapo Darajani, Desailly hakusita kumwagia sifa Terry, huku akisema kuwa ni mtu mwema anayependa kuwapa hamasa wachezaji ambao Conte huwa anawatumia katika kikosi chake cha kwanza.

“Ni mtu mwema kwa sababu huwapa hamasa wachezaji ambao Conte amewapanga kwenye kikosi cha kwanza, Kurt Zouma au Gary Cahill.”

0 comments:

Post a Comment