Wednesday, February 8, 2017

Rungu La TFF Latua Kwa Hemed Morocco

Kamati ya Bodi ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi imemfungia Kocha wa Stand United, Hemed Morocco kushiriki michezo mitatu uwanjani na faini ya Sh 500,000.

atika mechi Na. 160 ya Ligi Kuu ya Vodacom uliozikutanisha timu za JKT Ruvu na Stand United iliyochezwa Januari 30, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, Morocco aliondolewa kwenye benchi (Ordered off) kwa kosa la kupinga maamuzi ya mwamuzi na kutoa lugha chafu.

Kamati hiyo ya Saa 72 imechukua hatua hiyo kwa mujibu wa Kanuni ya 40 (11) ya Ligi Kuu kuhusu udhibiti wa Makocha.

Morocco hata kama atakuwa amemaliza mechi tatu nje ya benchi, hataruhusiwa kukaa kwenye benchi hadi awe amelipa faini hiyo.

Adhabu hiyo ya Morocco itaendelea kumhusu hata kama utakuwa umehamia kwenye timu nyingine na katika msimu mwingine wowote

Related Posts:

  • HIKI NDO KIKOSI CHA SERENGETI BOYS Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi amewataka wachezaji wa timu ya soka ya vijana wa Tanzania wenye umri wa chini ya miaka 17 maarufu kama jina la Serengeti Boys kwenda kucheza soka la ushi… Read More
  • TFF YAZIKUMBUSHA TENA KLABU ZA LIGI KUU 2016/17 Kwa mara nyingine, Bodi ya Ligi Kuu ya Shirikisho la Soka (TFF) imezikumbusha klabu zitakazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/17 kuwa mchakato wa wa utengenezaji kanuni umeanza tangu Mei 5, 2016. Bodi ya Ligi… Read More
  • SIMBA YAIFUATA MAJIMAJI SONGEA Kikosi cha Simba kimesafiri alfajiri ya leo kuelekea Songea tayari kwa mchezo wake dhidi ya Majimaji FC. Simba itaingia katika mchezo huu ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wake wa awali dhidi ya Mwadui FC, hivyo kuh… Read More
  • HASSAN RAMADHANI KESSY AMWAGA WINO YANGA Beki wa kulia wa Simba SC, Hassan Ramadhani Kessy (katikati) akitia dole gumba kwenye fomu za Mkataba wa Yanga, Kessy amesaini miaka miwili kuitumikia Yanga kuanzia mwezi ujao. Zoezi hilo lilifanyika juzi usiku mjini Dar… Read More
  • RATIBA YA FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO (ASFC) Fainali za kuwania Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) sasa zitafanyika Juni 11, 2016. Mchezo huo wa fainali utakaozikutanisha timu za soka ya Young Africans na Azam… Read More

0 comments:

Post a Comment