Sunday, February 5, 2017

Manchester City 2 - 1 Swansea City, Gabriel Jesus aipeleka city nafasi ya tatu EPL





Etihad Stadium
Manchester City imeitandika  Swansea City goli 2 -1 katika mchezo mkali na wakusisimua.
Kitu kizuri kwa Manchester city ni ujio wa mshambuliji Gabriel Jesus ambae ameongeza changamoto kwa Sergio Aguero katika nafasi ya upachikaji mabao.

Magoli yote miwili ya Manchester City yaliwekwa kimiani na Gabriel Jesus katika vipindi vyote viwili 11’ na 90’ wakati lile la kufutia machozi la Swansea limewekwa kimiani na Gylfi Sigurdsson 81’.

Mpka mwisho wa mchezo huo Manchester City iliibuka na ushindi huo na kuiwezesha kufikisha pointi 49 nyuma ya Totenham yenye pointi 50 na chelsea yenye pointi 59.
Kadi za njano

 Manchester City:   Kevin de Bruyne 41’ na Raheem Sterling 44,
Swansea City : Fernando Llorente 60’ , Jack Cork 74’ na Gylfi Sigurdsson 90’
                                     
     possession (%)

Manchester City:  69

Swansea City:     31

0 comments:

Post a Comment