Mchezo mmoja wakamilika huko Emirates Stadium na wenyeji
Arsenal wameibuka na ushindi wa 2 – 0 kwa
magoli ya Alexis Sanchez katika dakika 34 na 90(p).
Dakika ya 34 kazi nzuri ya Mesut Oezil iliokolewa na kumkuta
Kieran Gibbs ambae nae aliuelekeza mpira kimiani ila uhodari wa kipa aliweza
kuokoa mchomo huo na kumkuta Alexis Sanchez aliepiga tena ukaokolewa na
kumbabatiza mkononi na kuingia wavuni,
Goli la pili lilitokana na mpira wa penati ambayo mchezaji
wa Hully City Sam Clucas aliunawa kwa makusudi mpira uliopigwa na Lucas Perez,
na mwamuzi alimpa kadi nyekundu ya moja kwa moja na penati ilipigwa na Sanchez
na kuipatia timu yake uongozi wa 2 – 0.
Arsenal sasa imefikisha pointi 50 sawa na totenham iliyo
nafasi ya pili ila imezidiwa idadi ya magoli ya kufunga na kufungwa.
Mpka mwisho wa mchezo huo Arsenal 2 – 0 Hull City na kuzima ngebe
za hull city kuvitesa vilabu vikubwa.
kadi
Arsenal: Theo Walcott
53’ (Y), Kieran Gibbs 55’(Y) Alexis Sanchez 76’(Y)
Hull City: Andrea
Ranocchia 70’(Y) Sam Clucas 90’(R)
0 comments:
Post a Comment