Timu ya Genk
jana imeilaza timu inayoshika nafasi ya 11 ya Msimamo wa ligi kuu nchini
ubeligiji maarufu kama Belgium Pro League ya St.Truiden kwa jumla ya goli 3 – 0
katika dimba la Staaien.
Dakika ya 37
milango ya magoli ilianza kufunguliwa pale Alejandro Pozuelo alipomalizia kazi
nzuri kutoka kwa Siebe Schrijvers.
Dakika 2 (37’)
badae mtanzania Mbwana Ali Samatta aliiandikia timu yake goli la pili na goli lake 18 ndani ya kilabu hiyo na hivyo
kuvunja kabisa rekodi ya mchezaji wa Manchester City ya nchini England Kevin De Bruyne ya kuwa na goli 17 katika misimu yake
alipokuwa anaitumikia timu ya Genk.
Sasa Samatta
ankuwa ni mchezaji wa 14 wa miaka yote mwenye goli nyingi katika historia ya
kilabu ya Genk.
Dakika 45 Ruslan
Malinovsky alihitimisha karamu hiyo ya magoli pale alimalizia kazi ya Leandro
Trossard.
Mpaka mwisho
wa mchezo wenyeji St.Truiden 0 – 3 Genk, kwa Matokeo hayo Genk sasa imefikisha
pointi 41 baada ya michezo 26 huku kinara wa ligi hiyo akiwa ni Club Brugge
yenye pointi 52 baada ya michezo 25.
0 comments:
Post a Comment