Sunday, May 15, 2016

BARCELONA WATETEA UBINGWA WAO


Barcelona imetwaa ubingwa wa La Liga baada ya kuifunga Granada kwa jumla ya magoli 3 – 0 magoli yote yakifungwa na Luis Suarez, Barcelona wametwaa ubingwa huo kwa tofauti ya pointi 1 tu na mahasimu wao wakubwa Real Madrid ambao nao pia jana walishuka uwanjani kucheza na Deportivo mchezo ambao ulimalizika kwa Madrid  kushinda magoli 2 – 0 mabao yote yakifungwa na Christiano Ronaldo.

Licha ya kuisaidia timu yake kutwaa ubingwa huo Luis Suarez pia amemaliza msimu wa ligi akiwa kinara wa upachikaji wa magoli, akiwa na jumla ya magoli 40 akimuacha CR7 kwa tofauti ya magoli 5.

0 comments:

Post a Comment