Saturday, May 14, 2016

YANGA WAKABIDHIWA RASMI KOMBE LAO


KLABU Ya Yanga imekabidhiwa kombe lao jioni ya leo katika uwanja wa taifa mara tu baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Ndanda FC, mchezo ambao umemalizika kwa sare ya 2 - 2. Ndanda FC ndio walikuwa wa kwanza kupata goli kwa mkwaju wa penati dakika ya 29, goli ambalo limefungwa na Omary Mponda, lakini Yanga walifanikiwa kusawazisha goli hilo katika dakika ya 35 kupitia kwa Simon Msuva na dakika chache baadae dakika ya 41 Donald Ngoma akaongeza goli la pili, hadi timu zinakwenda mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa magoli 2 -1, kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kulisakama lango la Ndanda japo walishindwa kuzitumia vizuri nafasi nyingi walizozitengeneza, Ndanda walifanikiwa kusawazisha goli dakika ya 80 kupitia kwa mchezaji Salum Minely aliyeingia akitokea benchi. Hadi mpira unamalizika Ndanda FC 2 - 2 Yanga. 

Baada ya mechi hiyo ndipo Waziri wa Kilimo, Ufugaji na Uvuvi Mh. Mwigulu Nchemba ambaye ndo alikuwa mgeni rasmi katika mchezo wa leo aliwakabidhi Yanga kombe lao na sherehe za kufurahia taji hilo zikaanza rasmi.

0 comments:

Post a Comment