Majonzi yametawala katika nyuso za wapenda soka nchini baada
ya kuondokewa na Mzee Said Mohamed Abeid ambae ni mwenyekiti wa timu ya Azam
pia ni makamu mwenyekiti wa bodi ya ligi kuu Tanzania bara na mjumbe wa kamati
mbalimbali za shirikisho la soka Tanzania, TFF.
Mpaka umauti unamkuta alasir ya jana Novemba 7, 2016, na Mzee
Said Mohamed Abeid alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan ya jijini Dar
es Salaam.
Huko shinyanga ambapo timu ya Azam imekwenda kumalizia
mchezo wake wa mwisho dhidi ya Mwadui FC hali ya huzuni imetanda sana Miongoni mwa
wachezaji, benchi la ufundi, na viongozi wote walioambata na timu hiyo
Mzee Said atakumbukwa Kutokana na mchango wake mkubwa katika
kilabu ya Azam tangu kupanda daraja miaka 8 iliyopita, chini ya uongozi wake
Azam imeweza kutwaa makombe mbalimbali ikiwemo ligi kuu Tanzania Bara, Klabu
Bingwa Afrika Mashariki na Kati, mapinduzi cup.
Mzee Saidi atakumbukwa kwa uchesi,upendo, ukarimu na
uchapakazi wake katika soka la Tanzania.
Marehem alizaliwa visiwani Zanzibar mnamo tarehe 20 Machi
1940, amezikwa leo Jumanne ya tarehe 8 Novemba, 2016 kwenye makaburi ya Kisutu
baada ya swala ya saa kumi (Alasir).
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Mzee Said Mohamed
Abeid mahali pema peponi amiin
0 comments:
Post a Comment