Sunday, May 22, 2016

YUSUFU MANJI AWAPA MAGARI WACHEZAJI YANGA

Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusufu Manji ameahidi kuwapa magari wachezaji wa timu hiyo baada ya kufanikiwa kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika CAF, baada ya kuiondosha  Sagrada Esperanca ya Angola.





Manji amesema amefuraishwa na kitendo walichokifanya wachezaji wake kwani kimebeba utaifa na kupeperusha bendera ya Tanzania kupitia mchezo wa soka.

“Nataka kuwapa hamasa wachezaji wangu ili wafanye vizuri kwenye michuano hiyo ikiwezekana wafike fainali ya Kombe la Shirikisho na pia wabebe kombe la FA, dhidi ya Azam Jumatano uwanja wa taifa,” alisema mwenyekiti huyo wa klabu ya Yanga.

0 comments:

Post a Comment