Baraza la wazee la klabu ya Yanga hapo jana waliitisha mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya klabu.
Kaika mkutano huo ajenda kubwa ilikuwa ni gazeti linalomwandika vibaya mwenyekiti Yussuf Manji kuelekea uchaguzi mkuu wa klabu, wazee hao wamedai kuwa gazeti hilo linatumiwa na kikundi cha watu wachache wa Yanga ambao hawapendi mafanikio ambayo Manji anaipa Yanga.
Kikundi kinachoshutumiwa kulitumia gazeti hilo ni cha watu ambao walishawahi kuwa viongozi wa Yanga lakini hawakufanikiwa kuwapa Yanga maendeleo makubwa kama inavyoonekana hivi sasa chini ya Uongozi wa Manji.
Wakiongozwa na mzee Ibrahim Akilimali wazee hao waliwapongeza wachezaji wa Yanga,na kumshukuru Yussuf Manji kwa kuijenga Yanga yenye mafanikio na mshikamano huku wakiweka wazi kuwa wao wanamuunga mkono Manji kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
0 comments:
Post a Comment