Sunday, May 22, 2016

WANAOSUGUA BENCHI YANGA KUCHEZA NA MAJIMAJI LEO

Yanga imewasili Mjini Songea tayari kuvaana na Majimaji katika mchezo wao wa mwisho wa Ligi kuu Tanzania Bara.



Kuelekea mchezo huo Yanga imepeleka kikosi ambacho wengi wa wachezaji wake hawapati muda mwingi wa kucheza ukiachana na Deo Munish,Ally Mustafa na Joshua. 
Yanga imefanya hivyo kwa makusudi lengo likiwa ni kuwapumzisha wachezaji wake muhimu ili kukabiliana na na Azam FC katika mchezo wa  Fainali ya Kombe la shirikisho la TFF.

Wachezaji Waliobaki Dar ni Kevin Yondani, Thaban Kamusoko, Donald Ngoma, Vincent Bossou, Simon Msuva, Juma Abdul, Haruna Niyonzima, Amissi Tambwe, Benedictor Tinnoco na Malimi Busungu ambaye ni mgonjwa.

Walioenda kuivaa Majimaji ni Oscar Joshua ,Haji Mwinyi, Nadir Haroub,Benito John,Mbuyu Twite,Pato Ngonyani,Matheo Anthony,Deo Munishi,Ally Mustafa, na Paul Nonga.

0 comments:

Post a Comment