Ligi kuu Tanzania Bara Maarufu Vodacom ijatarajiwa kuendelea tena leo kwa mechi za mwisho za kufunga pazia la ligi hiyo.
Michezo itakayopigwa leo ni pamoja na Simba itakayokipiga na JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Azam FC ambayo inawania nafasi ya pili kama Simba, itakipiga na African Sports kwenye Uwanja wa AzamComplex, ulioko Chamazi, Mbagala nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.Mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga ya Dar es Salaam inakaribishwa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Majimaji mjini humo ilihali Mwadui na Kagera Stars zitamaliza ligi katika Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Kadhalika kwa mujibu wa ratiba hiyo ya Ligi Kuu ya Vodacom, Toto Africans itakuwa mwenyeji kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kuikaribishaStand United, wakati African Sports ‘Wanakimanumanu’ wameifuata Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Manungu, Mvomero mkoani Morogoro.
Mechi nyingine za kukunja jamvi kwenye Ligi Kuu ya Vodacom zitakuwa kati ya Mbeya City dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara huku mchezo mwingine wenye presha utakuwa ni kwa Tanzania Prisons yenye pointi 48 ambayo licha yakucheza na Coastal Union ambayo tayari imeshuka daraja kwenye Uwanja wa Mkwakwani, itakuwa inafukuziwa na Mtibwa Sugar kuwa na nafasi ya nne. Mtibwa Sugar ina pointi 47 na mvutano ni wa nafasi ya nne hasa ukirejea kwenye zawadi za Vodacom za Vodacom.
UNGANA NA SOKA24.BLOGSPOT.COM WAKATI WA MECHI HIZO KUPATA KILA KITAKACHOJIRI KATIKA VIWANJA HIVYO.
0 comments:
Post a Comment