Ripoti ya BBC imeeleza kuwa Manchester United wamepanga kumfukuza Louis van Gaal kesho Jumatatu na kumpa Jose Mourinho kibarua cha kuinoa United.
Louis Van Gaal ameiwezesha United kutwaa ubingwa wa FA, Man U wakitwaa taji hilo kwa Mara ya 12 sawa na Arsenal, Hata hivyo ubingwa huo haujaushawishi uongozi wa United kuendelea kubaki nae kwani wamepanga kutoa hatima yake Jumatatu hii.
BBC imeripoti kwamba Manchester United itamfukuza Van Gaal Jumatatu kabla ya kumtangaza Jose Mourinho baadaye wiki ijayo.
Alipohojiwa na waandishi wa habari baada ya mechi van Gaal Alisema "Nitawaonesha Kombe na sina muda wa kujadili mustakabali wangu na marafiki zangu wa vyombo vya habari ambao walinifukuzisha kazi tangu miezi sita iliyopita. Meneja gani anaweza kufanya nilichofanya?"
Van Gaal amekuwa akiishi kwa presha klabuni hapo tangu Jose Mourinho atimuliwe na Chelsea.
0 comments:
Post a Comment