Sunday, May 22, 2016

FUATILIA VITA YA KUSAKA NAFASI YA PILI KATI YA AZAM NA SIMBA HAPA SOKA24

Fuatilia Moja Kwa Moja Yote Yatakayojiri katia Michezo ya Timu Mbili zinazopigania nafasi ya pili kati ya Azam FC na Simba SC.




Ligi kuu Tanzania Bara inafungwa leo kwa timu zote kucheza katika kutamatisha ligi hiyo, Presha sasa imebaki katika sehemu 3 baada ya Yanga kuwa wameshatwaa ubingwa wa ligi hiyo, Kwanza wanaogombea nafasi ya pili, Azam FC na Simba SC, Wanaogombea nafasi ya 3, Mtibwa Sugar na Tanzania Prisons na Wanaopigana wasishuke Daraja, hawa ni African Sports ya Tanga yenye pointi 26 (nafasi ya 15); Mgambo pia ya Tanga iliyojikusanyia pointi 27 (nafasi ya 14); Kagera Sugar ya Kagera iliyovuna pointi 28 (nafasi ya 13); JKT Ruvu ya Pwani iliyopata pointi 29 (nafasi ya 12) na Toto Africans ya Mwanza yenye pointi 30 (nafasi ya 11).

Simba na Azam ambazo zina tofauti ya pointi moja katika msimamo wa ligi hiyo.  Azam FC ina pointi 63 ikishika nafasi ya pili nyuma ya mabingwa Yanga huku Simba inayoshika nafasi ya tatu ina pointi 62 hivyo kufanya kila mmoja hapa kumwombea mabaya mwenzie katika michezo ya leo.

Soka24 itakuletea yote yatakayokuwa yanajiri katika michezo hiyo hadi dakika za mwisho atakapojulikana nani amefanikiwa na nani amefeli.

0 comments:

Post a Comment