Bingwa mara sita wa michezo ya Olimpiki Usain Bolt ameandikisha muda wake bora zaidi msimu huu baada ya kutimka mbio za mita 100 nchini Jamhuri ya Czech.
Bolt alikimbia kwa chini ya sekunde 10 kwa mara ya kwanza, na kumaliza kwa sekunde 9.98 katika mashindano ya Golden Spike mjini Ostrava.Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kukimbia Ulaya mwaka huu, na alijikwamua baada ya kuanza vibaya kwa kumshinda Ramon Gittens.
Alimaliza mbele ya Gittens kwa sekunde 0.23.
Bolt anashikilia rekodi ya dunia katika mbio za 100m na 200m na kabla ya mbio hizo Ostrava alisema atalenga kuvunja rekodi ya dunia ya mbio za 200m mjini Rio mwezi Agosti.
Bolt alitumia sekunde 10.05 mbio zake pekee alizokimbia msimu huu, katika Cayman Islands Invitational Meet.
Mwanariadha huyo wa umri wa miaka 29 alipokea matibabu ya misuli ya paja baada ya mashindano hayo.
Alichukua likizo baada ya mashindano ya ubingwa wa riadha duniani jijini Beijing Agosti mwaka jana ambapo alishinda dhahabu katika mbio za 100m, 200m na 4x100m kupokezana vijiti.
0 comments:
Post a Comment