Tuesday, May 3, 2016

TFF WACHEZEA TENA RATIBA LIGI KUU TANZANIA BARA


Mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya Ndanda FC ya Mtwara na Yanga SC  itachezwa Mei 14, 2016 badala ya Mei 15, 2016 kama ratiba ya awali ilivyokuwa.
Bodi ya Ligi Kuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imerudisha mchezo huo Na. 218 utakaopigwa Uwanja wa Nangwanda Sijaona  Mtwara lengo likiwa  ni kuipa timu ya Young Africans nafasi ya kujiandaa na mechi yao itakayochezwa Angola  Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Sagrada Esperanca.
Mechi zingine zilizobadilishwa ratiba ni kati ya Simba na Mwadui ambayo sasa itachezwa Mei 8, 2016 badala ya Mei 7, 2016 sababu ikiwa ni kwamba Mei 7, 2016 kutakuwa na mchezo wa kimataifa utakaozikutanisha Yanga dhidi ya Sagrada Esperanca ya Angola.

Mchezo mwingine  ni kati ya Kagera Sugar dhidi ya Azam FC ambao sasa utafanyika Mei 8, 2016 badala ya Mei 7, 2016 sababu ikiwa ni kwamba Uwanja wa Kambarage Shinyanga. Mei 7, 2016 utakuwa na mchezo kati ya Stand United ya Shinyanga dhidi ya Coastal Union ya Tanga.

0 comments:

Post a Comment