Wednesday, May 4, 2016

ATLETICO MADRID YAIFUNGISHA VIRAGO BAYERN MUCHEN





Nusu fainali ya UEFA Champions ligi imeendelea Jana kwa mchezo mmoja ulowakutanisha Bayern Muchen ambao walikuwa nyumbani dhidi ya Atletico Madrid. Mchezo huo ulimalizika kwa Bayern kushinda magoli 2 - 1, hata hivyo Bayern wameondolewa katika michuano hiyo kwa goli la ugenini walilolipata Atletico kufuatia kushinda 1 - 0 katika mchezo uliopigwa Hispania Na goli moja ambalo wamelipata katika mchezo wa Jana, hivyo kufanya Aggregate kuwa 2 - 2.
Magoli yalifungwa Na Alonso dakika ya 31', Griezmann akasawazisha dakika ya 58' Na baadae Lewandowski akaifungia Bayern goli la pili kunako dakika ya 74'.
Mchezo mungine wa nusu fainali utapigwa Leo Kati ya Real Madrid wanaowakaribisha Manchester City.

0 comments:

Post a Comment