Friday, May 20, 2016

FIFA YAPELEKA SEMINA YA CLUB LICENSING ETHIOPIA

Wawakilishi wa Vilabu na Vyama Vya Mpira kutoka pande zote za Afrika watakutana Jijini Addis Ababa, Ethiopia wiki hii kwa ajili ya semina ya Club Licensing.



Wawakilishi wa Vilabu na Vyama Vya Mpira kutoka pande zote za Afrika watakutana Jijini Addis Ababa, Ethiopia wiki hii kwa ajili ya semina ya Club Licensing inayoendeshwa na Shirikisho la mpira wa miguu Duniani FIFA ikishirikiana na Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika CAF.

Lengo la semina hiyo ni kutekeleza mfumo wa Club Licensing duniani kote pamoja na kuzifanya klabu zijiendeshe kisasa zaidi katika nyanja zote zikiwemo kiufundi, kifedha na kiutawala. Semina hiyo itahusisha wawakilishi waandamizi kutoka nchini za Misri, Ethiopia, Gambia, Ghana, Kenya, Liberia, Libya, Nigeria, Somalia, South Afrika, Sudan na Tanzania katika kujulishana uzoefu  na kupeana njia bora za jinsi ya kuziendesha klabu kitaalam katika Afrika.

"Huu ni mpango mzuri unaowapa wanachama wote shiriki pamoja na vilabu, Ligi na wachezaji watakaohudhuria, zana za msingi zinazohitajika kutekeleza Club Licensing" alisema Salihu Abubakar Mtendaji Mkuu wa chama cha wachezaji wa kulipwa cha nchini Nigeria.

Nae Mkuu wa idara ya wachezaji wa kulipwa FIFA, James Johnson alisema, huu mfumo wa Club Licensing ulishaanza kufanya kazi na CAF huku vilabu 61 kutoka katika nchi 26 wakiwa wanachama.

Semina hiyo inakuwa ni mara ya pili kwa FIFA kufanya barani Afrika mwaka 2016.Uzinduzi wa Seminar hizi ulifanyika nchini Afrika Kusini na baadae seminar hizi zitafanyika nchini Morocco na Cameroon. Semina hizi pia zinafanyika katika maeneo mbalimbali duniani katika kipindi chote cha mwaka.

0 comments:

Post a Comment