Friday, May 20, 2016

MA SNIPER KULINDA MECHI YA UFUNGUZI EURO 2016

Ma-snjiper watatumika kulinda mechi ya ufunguzi michuano ya Euro 2016 kati ya wenyeji Ufaransa na Romania.



Ugaidi bado ni tatizo kubwa barani Ulaya na inaonekana wazi kuwa michuano ya Euro mwaka huu ndio tageti yao kubwa. Mechi ya Ufunguzi kati ya Ufaransa na Romania sambamba na mechi ya fainali ya michuano hiyo inahofiwa kuwa ndio michezo ambayo magaidi watafanya mashambulizi yao hii ni Kwa mujibu wa ripoti ya ofisi ya polisi inayoshughulika na makosa ya jinai ya nchini Ujerumani  (Bundeskriminalamt – BKA) iliyochapishwa katika gazeti la nchini humo.

Mechi hiyo ya Ufunguzi kati ya Ufaransa na Romania itachezwa June 10 katika uwanja wa Stade de France Stadium jijini Paris, moja kati ya miji ambayo inalengwa sana na magaidi. 

Shirikisho la Mpira wa miguu barani Ulaya UEFA limepanga kupeleka maaskari 10,000 kwenda kuimarisha ulinzi katika michezo yote itakayochezwa katika michuano hiyo lengo likiwa kila mechi moja ilindwe na askari 900.

Related Posts:

  • Mengine Yakustaajabisha Yanayomhusu Neymar Jr Ni mara chache sana hutokea mtu  kumsikitikia mchezaji Mkubwa anaepata kipato kidogo, lakini habari zilizovuja hivi punde kupitia mtandao wa Football Leaks zinaonyesha kwamba Neymar anapata Sh. Milioni 240 kw… Read More
  • Mnyama Afanyiwa Ujangili TaifaTimu ya soka ya Simba SC imejikuta nje ya michuano ya FA baada ya kupokea kichapo toka kwa timu ya Coastal Union. Katika mchezo huo wa vuta nikuvute Coasta ilikuwa yakwanza kutikisa nyavu za Simba baada ya mchezaji Yusuf kupi… Read More
  • Matokeo Ya UEFA Champions League Jana Jumanne UEFA Champions League imeendelea tena jana kwa mechi mbili zilizozikutanisha timu za Real Madrid vs Wolfsburg na Manchester City vs PSG. katika mechi hizo timu za Real Madrid Na Manchester City ya Uingereza zimefanikiwa … Read More
  • Adam Johnson Kukata Rufaa Mchezaji Adam Johnson amefikia maamuzi ya kukata rufaa kufuatia sakata lake la kufanya mapenzi na binti mwenye umri wa chini ya miaka 18, Johnson ameamua kufikia maamuzi hayo baada ya hukumu yake ya kifungo cha… Read More
  • "Mapema Sana Kumwita Van Gaal Failure" Jordi Cruyff Van Gaal Nyota wa Zamani wa Barcelona na Manchester United Jord Cruyff amewabeza wanaomponda kocha wa Manchester United Louis Van Gaal kwa kuwaambia ni mapema sana kumwona kocha huyo ni failure (aliefeli ). Jord ali… Read More

0 comments:

Post a Comment