Ufaransa na Ujerumani zimetoa angalizo kwamba kikundi cha kigaidi cha ISIS kinapanga kufanya mashambulizi katika michuano ya Euro 2016
Katika mataifa yote yatakayoshiriki Euro 2016 Ufaransa pekee ndiyo inakuwa katika hofu kubwa ya kushambuliwa na kundi la IS. Afisa mkuu wa upelelezi nchini humo Patrick Calvar ameliambia bunge la nchini hiyo juu ya tishio hilo. Ufaransa inakuwa katika hofu kubwa ya kushambuliwa kutokana na michuano ya Euro 2016 inayotarajiwa kutimua vumbi mapema mwezi ujao katika nchi hiyo.
"Inafahamika wazi kuwa Ufaransa ndio nchi inayolengwa na magaidi kwa sasa na kikundi cha kiislam cha Islamic State kinapanga kufanya mashambulizi" alisema Calvar, "kutokana na mateso wanayoyapata katika uwanja wa vita huko Iraq na Syria, ISIS watataka kulipiza kisasi"
"watataka kushambulia mapema sana iwezekanavyo ili kutimiza lengo lao, huu utakuwa muundo mpya wa mashambulizi utakaohusisha kutega vifaa vya milipuko katika maeneo ambayo watu wengi watakuwa wanakusanyika". aliongeza Calvar.
Hata Hivyo Calvar alisema vikosi vya ulinzi vimeimarishwa kuhakikisha mashindano yanafanyika kwa salama na amani.
0 comments:
Post a Comment