Friday, May 20, 2016

YANGA; "KOMBE LA UBINGWA LIGI KUU HALINA HADHI"

Ofisa habari wa klabu ya Yanga Jerry Muro amelikosoa kombe la ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara kwa kusema halina Hadhi.



Akizungumza na waandishi wa Habari jana Muro alisema kombe hilo halina hadhi ukilinganisha na ukubwa wa ligi kuu, hivyo kuwaomba TFF pamoja na mdhamini wa ligi kuu kufanya marekebisho ya kombe hilo, Muro aliongeza kwa kusema kombe la Azam Sports Confederation Cup maarufu kama kombe la FA lina mwonekano mzuri na ni zuri ukilinganisha na ligi kuu.

“Lile kombe kwa kweli halina hadhi, lina michubuko kibao," alisema Muro.
Kombe analopewa bingwa wa ligi kuu Tanzania Bara

“Hivyo nawashauri TFF na wadhamini wetu wa ligi ni vema wakariboresha kombe hilo, pia ni lazima liwepo moja litakalofanana na siyo kubadilishwa kila msimu" aliongeza Jerry Muro.
Kombe atakalopewa Bingwa wa FA Cup

Yanga imechukua kombe hilo mara ya 26 tangu kuanzishwa kwa klabu hiyo mwaka 1935.

Related Posts:

  • KIMESHAELEWEKA YANGA WAPYA WOTE RUKSA ISIPOKUWA HUYUWachezaji wote wapya wa Yanga wamethibitishwa kuwa huru kuanza kuitumikia klabu hiyo isipokuwa Hassan Ramadhan Kessy. Yanga imewasajili wachezaji watano hadi sasa ambao ni Andrew Vicent, Juma Mahadhi, Ben Kakolanya, Hassan… Read More
  • KUMBE HIKI NDO KINACHOITAFUNA SIMBAKumekuwa na madai kwamba kuna kiongozi mmoja ndani ya klabu ya Simba kuwa anaihujumu klabu hiyo katika ligi kuu Vodacom. Rais Wa Simba Evans Aveva Uongozi wa klabu ya Simba umeamua kulivalia njuga suala hilo ili kubaina n… Read More
  • TFF YAJA JUU SUALA LA KESSYShirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limesema litaingilia kati suala la mchezaji Ramadhan Kessy aliyesajiliwa na Yanga huku Simba wakikataa kuiandikia barua Yanga kumruhusu mchezaji huyo kuanza kuitumikia klabu hiyo. … Read More
  • SHOMARI KAPOMBE KURUDI MSIMBAZIKlabu ya Simba imesema inapambana kuhakikisha wanamrudisha kikosini beki wao Shomari Kapombe anayeitumikia klabu ya Azam FC kwa sasa. Kapombe ambaye hivi karibuni ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa msimu uliopita ligi kuu Vo… Read More
  • SIMBA WAZIDI KUWEKA NGUMU KWA YANGA KUHUSU KESSYKlabu ya Simba imesema kama si Yanga kuwapatia fedha hawataandika barua itakayomuidhinisha Hassan Ramadhan Kessy kucheza michuano ya Kombe la shirikisho CAF CC Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa kamati ya Usajili wa Simba, Za… Read More

0 comments:

Post a Comment