Saturday, May 28, 2016

KRC GENK WAMZUIA SAMATTA KUJIUNGA NA TAIFA STARS

Klabu ya Genk anayocheza Mfungaji bora wa Afrika mwaka 2015, Mtanzania Mbwana Ally Samatta imemuombea mchezaji huyo kutoungana na timu yake ya taifa katika mechi ya kirafiki na Kenya.




Mbwana Samatta ataikosa mechi kati ya Taifa Stars na Kenya baada ya klabu yake kuomba kwa Shirikisho la mpira Tanzania kumwachia mchezaji huyo ili aweze kuisaidia timu yake ya Genk katika mchezo wa mwisho wa kuwania nafasi ya kushiriki michuano ya Europa msimu ujao.

Genk imeomba Samatta abaki katika klabu yake ili atoe mchango wake katika mechi hiyo muhimu ambayo endapo Genk watafanikiwa kushinda basi itakuwa imekata ticket ya kushiriki michuano ya Europa league msimu wa 2016/17. 

Mchezo kati ya Tanzania na Kenya ni wa kujiandaa na mechi na Misri katika kuwania kufuzu kombe la mataifa ya Afrika AFCON.

Kikosi kilichoitwa na kocha Mkwasa ni Deogratius Munish, Aishi Manula na Benny Kakolanya (Makipa).

Mwinyi Haji, Juma Abdul, Aggrey Moris, David Mwantika, Erasto Nyoni, Mohamed Hussein na Vicent Adrew (Mabeki).

Viungo ni Himid Mao, Farid Mussa, Jonas Mkude, Mwiny Kazimoto, Mohamed Ibrahim, Shiza kichuya, Ismail Issa, Juma Mahadhi na Hassan Kabunda. Wakati Washambuliaji ni Elias Maguli, Ibrahim Ajib, Mbwana Samatta, Jeremiah Juma, John Bocco na Deus Kaseke.

0 comments:

Post a Comment