Friday, May 27, 2016

ERICK MAWALLA AISHITAKI MBEYA CITY TFF

Shirikisho la Mpira Miguu nchini TFF, limepokea mashitaka kutoka kwa aliyekuwa mchezaji wa Mbeya City Erick Mawalla kwa kushindwa kumlipa pesa za usajili na mishahara zaidi ya Sh. milioni 10.



Mawalla amesema aliondolewa katika kikosi cha Mbeya City tangu mwaka jana baada ya aliyekuwa kocha wa City Meja Mingange kutokuwa na Mipango nae.

"Katibu (Emmanuel Kimbe) ndiye aliyenipigia simu kuwa sihitajiki kwenye timu, kocha hakuwa na mipango na mimi, niliomba nipewe barua lakini hakunipa zaidi ya kuniambia nitafute timu nyingine, kikubwa hata mshahara wangu nimeingiziwa kwa mara ya mwisho Oktoba mwaka jana. Hivyo nadai pesa ya Usajili na mishahara tangu kipindi hicho;" alisema Mawalla alipohojiwa na gazeti la Mwanaspoti.

Aidha Mawala amesema alishawaandikia barua ambayo kwa madai yake aliwapa muda wa wiki 2 wawe wamempa ufafanuzi juu ya mustakabali wake lakini hajajibiwa.Kutokana na hali hiyo na kutokupokelewa kwa simu zake anapowapigia viongozi wa Mbeya City ndipo Mawalla alipoamua kukimbilia TFF ili watoe mwongozo wa jambo hili ikiwezekana yeye apate haki yake.

0 comments:

Post a Comment