Friday, May 27, 2016

NADIR HAROUB AMTOLEA NJE MAZIMA MKWASA KUJIUNGA NA TIMU YA TAIFA

Mchezaji Mkongwe wa timu ya Yanga na Taifa, Nadir Haroub maarufu kama Cannavaro, amekataa kabisa kujiunga na timu ya Taifa itakayocheza dhidi ya Kenya katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki.



Cannavaro amesema hawezi kuitikia wito huo kwa kuwa tayari yeye alishaandika barua ya kuacha kuitumikia timu ya Taifa na kuelekeza nguvu zake katika klabu yake ya Yanga.

"Naheshimu uteuzi wa Kocha Mkwasa na pia nafurahi kuona jina langu miongoni mwa majina 26 ya wachezaji walioitwa kwenye kikosi cha Stars, lakini haitakuwa rahisi kwangu kurudi kuichezea timu hiyo kwasababu nilishatangaza kustaafu na barua niliiandikia shirikisho (TFF),naomba kocha anisamehe kwa hilo" alisema Cannavaro.

Nadir alitangaza kuacha kuitumikia timu ya taifa baada ya Mkwasa kumvua unahodha wa timu hiyo na kumpa Mbwana Samatta bila kumjulisha kabla ya uamuzi wake huo, kitendo ambacho Cannavaro hakukifurahia.

0 comments:

Post a Comment