Hans Pope bosi anayeshughulikia maswala ya Usajili kunako klabu ya Simba ameweka bayana kuvutiwa kwake na Mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma.
Hans Pope amesema licha ya Amiss Tambwe kuibuka Mfungaji bora katika msimu wa ligi uliomalizika hivi karibuni kwake yeye anawakubali wachezaji wawili tu. Akizungumza na Gazeti la Mwanaspoti Hans alisema mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma na Kiungo wa Simba Justice Majabvi ndio wachezaji pekee anaowakubali kutokana na uwezo wao mkubwa wanapokuwa uwanjani, Huku akisisitiza kwamba Ngoma ndiye Mkali zaidi ya wote.
"Simba bila wasiwasi nitamtaja Majabvi, amekuwa na msaada mkubwa sana katika timu yetu lakini nje ya Simba kwa Azam namuona Kipre Tchetche yuko vizuri." alisema Hans Pope.
"Lakini Ukiangalia kwa Ujumla yule Mshambuliaji wa Yanga, Ngoma amekuwa kivutio kikubwa, ni mchezaji anayeweza akatengeneza goli la kwake si aina ya washambuliaji ambaye anaweza kutegemea mipira ya kulishwa" aliongeza Hans Pope.
Simba imemaliza ligi katika nafasi ya tatu na Hans Pope kama bosi wa kamati ya Usajili klabuni hapo ameshawahi kupitia wakati mgumu katika ligi kuu Msimu huu pale mashabiki walipokamzingira wakionyeshwa kukerwa kwao na muenendo wa timu yao pale Simba ilipofungwa na Toto Africans katika mchezo wa ligi msimu huu. Kutokana na hali hiyo Uongozi wa Simba kwa sasa unahaha kutafuta wachezaji wazuri watakaoimarisha sawasawa kikosi chao tayari kwa kuleta ushindani mkubwa katika msimu ujao wa ligi.
0 comments:
Post a Comment