Saturday, April 16, 2016
TFF Yatuma Salamu Za Rambirambi MZFA
Shirkisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetuma salamu za rambirambi kwa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Mwanza (MZFA), kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti mstaafu wa MZFA na makamu mwenyekiti wa FAT Silvanus Makalu Ngofilo aliyefariki dunia juzi jijini Mwanza.
Katika salamu zake, TFF imewapa pole familia ya marehemu Ngofilo ndugu, jamaa, marafiki, wadau wa mpira wa miguu kanda ya Ziwa na kusema Shirikisho liko pamoja nao katika kipindi hiki cha maomblezo.
Mazishi ya Silvanus Makalu Ngofilo yatafanyika kesho Jumapili kijijini kwao Mwamanyili, Wilayani ya Busega mkoa wa Shinyanga ambapo TFF itawakilishwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Vedasto Lufano.
Marehemu Ngofilo wakati wa uhai wake aliwahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa FAT wakati wa Muhidin Ndolanga na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya FAT, Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Mwanza (MZFA) 1984-1994, ambapo baada ya kustaafu alipewa wenyekiti wa heshima na MZFA.
Related Posts:
HONGERENI AZAM FC KWA HILI MNALOLIFANYA Azam FC inawakaribisha vijana wote Tanzania mwenye umri chini ya miaka 20 yani (U-20), nenda kajaribu bahati yako ya kufanya majaribio na kujiunga na 'Azam FC Academy' Jumamosi hii Mei 7 ndani ya makao makuu y… Read More
RUFAA HIZI 8 KUTOLEWA MAAMUZI NA KAMATI YA RUFAA YA NIDHAMU TFF KESHO Kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kesho Jumanne Mei 3, 2016 saa 5:00 asubuhi itatangaza uamuzi wa rufaa nane zilizowasilishwa na kujadiliwa za viongozi, mchezaji na timu tatu zilizoshiriki … Read More
HAMISI TAMBWE AIFIKIA REKODI YA ABDALLAH JUMA YA MWAKA (2006) Mshambuliaji wa Klabu ya Yanga Hamisi Tambwe ndiye anaongoza katika chati ya ufungaji bora ligi Kuu Tanzania bara Msimu huu wa 2015/2016. Tambwe ambae jana alifunga goli katika mechi dhidi ya Stand United, alifikisha jum… Read More
TFF WACHEZEA TENA RATIBA LIGI KUU TANZANIA BARA Mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya Ndanda FC ya Mtwara na Yanga SC itachezwa Mei 14, 2016 badala ya Mei 15, 2016 kama ratiba ya awali ilivyokuwa. Bodi ya Ligi Kuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imerudisha mchezo… Read More
UCHAGUZI MKUU YANGA WASOGEZWA MBELE Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imetangaza Uchaguzi Mkuu wa Klabu ya Yanga kuwa utafanyika Juni 25, 2016 badala ya Juni 5, 2016. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imelazimika kufanya hivyo kwa kuzingat… Read More
0 comments:
Post a Comment