Friday, May 6, 2016

HAWA NDO WAAMUZI WA MECHI YA YANGA NA ESPERANCA


Mwamuzi Joseph Odartei Lamptey, Jumamosi Mei 7, 2016 anatarajiwa kuwa mwamzi wa kati katika mchezo wa kimataifa kuwania Kombe la Shirikisho Barani Afrika utakaozikutanisha timu za Young Africans ya Dar es Salaam, Tanzania na GD Sagrada Esperanca ya Angola.

Lamptey kutoka jiji la Accra, Ghana atasaidiwa na raia wenzake wa nchi hiyo kuchezesha mchezo huo Na. 99. Mwamuzi Msaidizi Na. 1 (line 1) ni David Laryea wakati Mwamuzi Msaidizi Na. 2 (line 2) ni Malik Alidu Salifu.

Mwamuzi Msaidizi mezani (Fourth Official) ni Cecil Amately Fleischer huku Kamishna wa mchezo huo, akiwa ni Asfaw Luleseged Begashaw wa Ethiopia.

Viingilio na upatikanaji wa tiketi utatangazwa leo Ijumaa Mei 6, 2016 na uongozi wa klabu ya Young African mara baada ya mkutano kati ya makocha wa timu zote mbili. Mkutano wa makocha hao utafanyika saa 5.00 mchana kwenye Ukumbi wa mikutano wa TFF.


Related Posts:

  • CAF YAISAFISHIA NJIA YANGAShirikisho la mpira wa miguu Afrika (CAF), limemthibitisha beki Hassan Kessy kuichezea Yanga katika michuano ya Kombe la CAF CC katika hatua ya makundi. Caf pia imetuma leseni ya wachezaji wengine watatu wa Yanga walioonge… Read More
  • STAND UNITED YAISHITAKI SHIREFA TFFUongozi wa Stand United, umeliomba shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF kukemea kitendo cha uongozi wa chama cha soka Mkoani Shinyanga (SHIREFA) kuandikisha wanachama wa klabu hiyo wakati kuna viongozi. Mwenyekiti wa … Read More
  • KIFAA KIPYA YANGA KUTUA LEO JANGWANIWalter Musona Mshambuliaji kutoka FC Platinum ya Zimbabwe anatarajiw kuwasili Daresalaam leo alasiri kwa ajili ya mazungumzo na klabu ya Yanga. Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika kutoka katika klabu ya Yanga, tayari mambo yo… Read More
  • MATARAJIO YA SIMBA KIKOSI KIPYA MSIMU UJAOZacharia Hans Poppe, mwenyekiti wa kamati ya usajili Simba, amesem a kikosi chao msimu ujao kitakuwa na mabadiliko makubwa kuanzia benchi la ufundi hadi wachezaji. Simba kwa sasa ipo katika harakati za kuhakikisha wanawana… Read More
  • KASEKE ACHEKELEA MAISHA YANGAKiungo wa Yanga, Deus Kaseke amesema anajiona ni mwenye bahati kwa kufanikiwa kuchukua mataji mawili (Ligi kuu Vodacom & Kombe la FA) pamoja na kucheza hatua ya makundi kombe la shirikisho Afrika CAF CC katika msimu wake … Read More

0 comments:

Post a Comment