Friday, May 6, 2016

HABARI 5 KUBWA ZA USAJILI LEO IJUMAA MAY 6, 2016


Pep Guardiola Anamtaka Arteta Man City
Midfielder huyo anategemewa kuondoka katika klabu ya Arsenal mwisho mwa msimu huu, ambapo mkataba wake na Arsenal unamalizika, baada ya miaka 5 ya kuitumikia Arsenal na tayari ameshapewa ofa ya kujiunga na Man City.

Mahrez Anataka Kubaki Leicester City
Mchezaji wa kimataifa wa Algeria Riyad Mahrez anawindwa na vilabu vingi vikubwa barani ulaya, lakini yeye mwenyewe amewaambia viongozi wa Leicester kuwa anataka kubaki katika uwanja wa King Power na mabingwa hao wapya.

Flamini Apewa Ofa na Klabu Ya Panathinaikos
Timu hiyo ya Ugiriki imedhamiria kuinasa saini ya Midfielder wa The Gunners, Flamini kufuatia Mkataba wa mchezaji huyo kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

Chelsea Wavutiwa Na Morata
Klabu ya Juve ipo tayari kumuuza Morata kwenda klabu ya Chelsea endapo watakubaliana kiasi cha pesa kitakachotajwa.

Arsenal Waisaka Saini Ya Kante

Klabu ya Arsenal imekuwa na mazungumzo ya mara kwa mara na wakala wa Midfielder huyo wa Leicester City, hizo zikiwa ni harakati za Wenger kukiboresha zaidi kikosi chake.

0 comments:

Post a Comment