Sunday, April 10, 2016

Barcelona Yapokea Kichapo Dhidi Ya Sociedad


Barcelona imekutana na kipigo cha bao 1-0 ikiwa ugenini dhidi ya Real Sociedad ambayo ilicheza vizuri katika kipindi cha kwanza na kupata bao kupitia Kimel Oiarzabal katika dakika ya 5.
Jitihada za Lionel Messi na Neymar kutaka kusawazisha ziligonga mwamba hadi mpira unamalizika. Matokeo haya yanaiweka Barcelona katika nafasi ile ile ya kwanza ikiwa imetofautiana kwa point tatu tu na Atletico Madrid inayoshika nafasi ya pili huku Real Madrid ikiwa katika nafasi ya Tatu kwa tofauti ya pointi 4 na Barcelona
Ndani ya mechi tatu, imepoteza mbili baada ya kuchapwa na Real Madrid kwa mabao 2-1, ikaamka na kuitwanga Atletico Madrid 2-1 kabla ya kukutana na kipigo cha leo.

0 comments:

Post a Comment