Wednesday, June 8, 2016

TAYARI MOURINHO AMEMNASA ERIC BAILLY WA VILLARREAL

Eric Bailly anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Jose Mourinho katika klabu ya Manchester United.


Eric Bailly amekamilisha vipimo vya afya mapema leo na tayari beki huyo ameshasaini mkataba wa miaka 4 na klabu ya Man U.
Bailly 22, ni raia wa Ivory Coast na amesajiliwa na United kwa kitita cha paundi milioni 30.

Baada ya dili hilo kukamilika Bailly aliyasema haya;

"Ndoto yangu imetimia kujiunga na Manchester United. Kucheza mpira katika level za juu ni kitu ambacho nimekuwa nakihitaji siku zote".

Mourinho naye alisema " Eric anauwezo utakaomfanya kuwa mmoja kati ya wachezaji bora".

Bailly amecheza mechi 40 katika ligi kuu nchini Hispania, La Liga, mechi tano za kwanza kati ya hizo amecheza akiwa na klabu ya Espanyol.

Alijiunga na Villarreal kwa uhamisho wa paundi milioni 4.4, Januari 2015 na alicheza kila mechi.

Bailly anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Mourinho huku pia akisubiriwa Zlatan Ibrahimovic kuungana na Mourinho katika Dimba la Old Trafford.

0 comments:

Post a Comment