Thursday, March 23, 2017

FERGUSON: Ronaldo na Messi, wakizeeka Soka la hispania litadorora


Kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson anaamini soka la Hispania litakoma kutawala ulaya katika ngazi ya vilabu.

Katika kipindi cha miaka nane iliyopita vilabu vya Hispania vimetwaa kombe la ligi ya mabingwa ulaya ‘UEFA Champions league’ mara 5, achilia mbali kombe la EUROPA ambapo Sevilla imelichukua mara tatu mfululizo katika miaka hiyo.

Sir Alex Ferguson amesema kuwa vilabu vya nchi Fulani kuwa na mafanikio huwa ni kipindi cha mpito na akatoa mifano ya wazi.

Mfano miaka ya1970  Ajax na Bayern Munich ndio walikuwa vinara wa kubeba kombe hilo, miaka ya 1980 ikawa zamu ya Liverpool , miaka 1990 Italy na AC Milan walitwaa zaidi kombe hilo wakati.
Pia hakusita kuitaja Manchester United katika kipindi cha miaka 4 ndani ya miaka sita iliyopita Manchester ilicheza fainali tatu.

“Naamini sasa ni zamu ya vilabu vya Hispania kutawala, ni timu bora na ndio maana zinatawala. Lakini mambo yatabadilika kama yanavyobadilika, unajua Ronaldo na Messi watazeeka, je nani m’badala wao? Hivyo nadhani mzunguko utaendelea. ”

Vilabu vitatu vya Hispania vimefuzu katika hatua ya Robo fainali ya ligi ya mabingwa, vilabu hivyo ni bingwa mtetezi wa kombe hilo Real Madrid, Barcelona na Atletico Madrid.
Real Madrid itakutana na Bayern Munich
Barcelona watakutana na Juventus

Atletico Madrid watakutana na Leicester City.

0 comments:

Post a Comment