Tottenham Na Arsenal Wanasaka Saini Ya Midfieda Wa Southampton Victor Wanyama
Wanyama alikuwa karibu kujiunga na Tottenham msimu uliopita lakini dili hilo lilifeli. Inasemekana Spurs bado wanania ya kumsajili Wanyama wakati Arsenal nao wakimfuatilia kwa ukaribu. Ripoti kutoka Sky Sports zinasema Wanyama anataka kuondoka klabuni hapo baada ya kukataa kuongeza mkataba wa miaka 5 mwezi september mwaka jana.
Kocha wa Spurs Mauricio Pochettino alimsajili Wanyama wakati huo akiwa kocha wa Southampton na sasa anataka kumtoa Southampton na kumleta Spurs kutokana na kuvutiwa na kiwango chake.
Arsenal wapo katika harakati za kuwapata Midfielders wapya katika kikosi chao baada ya kuwaruhusu Mikel Arteta, Tomas Rosicky na Mathieu Flamini kuondoka klabuni hapo na Victor Wanyama amewekwa katika orodha ya wanaowindwa na klabu hiyo.
0 comments:
Post a Comment