Thursday, May 19, 2016

RAIS WA CAF ATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI CAMEROON

Rais wa shirikisho la Mpira wa miguu barani Africa Issa Hayatou ametuma salam za rambirambi Cameroon kufuatia kifo cha David Mayebi



katika barua ya tarehe 18 Mei 2016 iliyotumwa kwa rais wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Cameroon (FECAFOOT), rais wa shirikisho la Mpira wa miguu barani Afrika Issa Hayatou amesema amepokea kwa huzuni kubwa taarifa za kifo cha David Mayebi kilichotokea Mei 15, 2016 huko Yaounde baada ya kuugua.

"Katika wakati huu wa majonzi, napenda kutoa pole kwa niaba ya kamati nzima ya utendaji CAF kwa Familia ya wanamichezo wote Afrika, na wakameruni wote waliofikwa na msiba huo" aliandika rais wa CAF katika barua yake. 

Mayebi amewahi kuwa mchezaji wa kimataifa wa Cameroon, alizaliwa Novemba 10 mwaka 1954 na ameshawahi kufanya kazi ya ukocha baada ya muda wake wa kucheza soka kumalizika.
David Mayebi Enzi Za Uhai Wake

Baada ya kushiriki katika kuunda chama cha wanasoka wa Cameroon (Association of the Cameroonian Footballers-AFC) ambacho alikuwa rais wa chama hicho, Mayebi pia amewahi kuwa mjumbe wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Cameroon na alipata kuwa makamu wa rais wa shirikisho hilo mara moja.

Kimataifa; Mayebi alikuwa Mjumbe wa bodi ya Shirikisho la kimataifa la wachezaji wa kulipwa (Federation of Professional Footballers-FIFPro)

Mungu Ailaze Mahala Pema Roho Ya David Mayebi-Ameen

0 comments:

Post a Comment