Friday, May 13, 2016

ZLATAN IBRAHIMOVIC ATANGAZA RASMI KUONDOKA PSG


Paris: Zlatan Ibrahimovic amethibitisha ijumaa hii kuwa ataihama klabu ya Paris Saint-Germain mwishoni mwa msimu huu wa ligi, lakini Uongozi wa mabingwa hao wa ligi kuu nchini Ufaransa ligue 1 wamesema nyota huyo atarudi tena katika klabu hiyo hapo baadae na atapewa majukumu ya kiutawala.

“Mechi yangu ya mwisho katika uwanja wa Parc des Princes ni kesho. Nimefika katika klabu hii kama mfalme na naondoka kama Legend”. Yalikuwa maneno ya Ibrahimovic huku akimaliza uvumi kuwa huenda angeongeza mkataba wake na klabu hiyo mara baada ya mkataba wake wa sasa kumalizika.

Ibrahimovic ambaye mkataba wake na PSG unamalizika June 30 mwaka huu, atacheza mechi yake ya mwisho wa msimu dhidi ya Nantes jumamosi hii.
Wote wameshakubaliana kuwa mara baada ya Ibrahimovic kuacha kucheza soka, basi atajiunga na klabu hiyo tena kama kiongozi wa timu na si mchezaji.

Ibra anahusishwa na kujiunga na klabu za ligi kuu nchini Uingereza wakati huo wakala wake akisema kwamba superstaa huyo huenda akajiunga na timu yake ya zamani ya AC Milan.

Ibrahimovic ambaye wikiendi iliyopita alipewa taji la mchezaji bora wa mwaka Ufaransa kwa mara ya 3, amefurahia mafanikio makubwa aliyoyapata akiwa klabuni hapo tangu ajiunge na miamba hiyo ya Ufaransa akitokea AC Milan mwaka 2012, ameshinda taji la ligi kuu nchini humo katika misimu yote 4 aliyotumikia klabuni hapo, na endapo PSG watashinda kombe la Ufaransa (French cup) wiki ijayo basi PSG watakuwa wametwaa mataji yote ya ndani huku Ibrahimovic akishinda jumla ya makombe 12 tangu ajiunge  na klabu hiyo.

Related Posts:

  • STUTTGART 3 ZASHUKA DARAJA MSIMU HUU Msimu wa ligi wa 2015/16 umekuwa msimu mbaya kwa wakazi wa jiji la Stuttgart  katika tasnia ya mpira wa miguu. Timu tatu za Stuttgart zimeshuka daraja katika ligi zote 3 zikizoshiriki, Stuttgart iliyokuwa inashiriki… Read More
  • ZLATAN IBRAHIMOVIC ATANGAZA RASMI KUONDOKA PSG Paris: Zlatan Ibrahimovic amethibitisha ijumaa hii kuwa ataihama klabu ya Paris Saint-Germain mwishoni mwa msimu huu wa ligi, lakini Uongozi wa mabingwa hao wa ligi kuu nchini Ufaransa ligue 1 wamesema nyota huyo atarudi… Read More
  • WAZIRI WA KILIMO KUWAKABIDHI YANGA KOMBE LAO LEO Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba Madelu leo Jumamosi Mei 14, 201 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Ndanda na Young Africans  mchezo utakaofanyi… Read More
  • SIR ALEX FERGUSON AKIRI KUFANYA KOSA KUBWA UNITED Sir Alex Ferguson amekiri waziwazi kuwa maamuzi yake ya kutangaza kuwa angestaafu mwaka 2001 lilikuwa ni kosa kubwa katika maisha yake ya ukocha. Kocha huyo wa zamani wa Man Utd Sir Alex Ferguson alikaa klabuni hapo k… Read More
  • ARSENE WENGER KUSAINI MKATABA MWINGINE NA ARSENAL Uongozi wa klabu ya Arsenal umepanga kumwongeza mkataba wa miaka 2 kocha wake Arsene Wenger mkataba ambao anatarajiwa kusaini October mwaka huu, lengo likiwa ni kupata muda wa kutosha wa kumtafuta atakaekuwa mrithi wa We… Read More

0 comments:

Post a Comment