Ni hatua nzuri katika maisha yake ya soka, akiwa ametumikia klabu ya Aminens kwa miaka mitatu na kufanikiwa kupewa jukumu la unahodha katika kikosi cha vijana U17s, sasa hivi amepata mkataba wake mkubwa.
Ikiwa inashika nafasi ya 8 katika msimamo wa ligi kuu nchini Ufaransa Ligue 1, Caen wameonyesha uwezo mkubwa katika ligi hiyo.
Baada ya kumuuza N’Golo Kante katika klabu ya Leicester City msimu uliopita, Caen walikuwa mawindoni kusaka kiungo mkabaji ambaye anaweza akakaba na kushambulia kwa wakati mmoja na Yaya Toure ameonekana kufiti katika nafasi hiyo, kutokana kuwa na kiwango kinachoonekana kufanana na cha Kante.
Amepewa jezi namba 6, namba ambayo alikuwa akiivaa pia alipokuwa na klabu ya Amiens, Yaya alitangazwa rasmi na Caen kuwa ni mchezaji wa timu hiyo kwa sasa.
Kiungo huyo mkabaji anafanana jina na midfielder wa Manchester City Yaya Toure, lakini licha ya kuwa na majina yanayofanana hakuna uwezekano wa kuwachanganya kwa kutokujua yupi ni yupi.
0 comments:
Post a Comment